Important Dates
37th Swahili Colloquium
Friday, 30.05.2025- Sunday, 01.06.2025
Iwalewahaus, Bayreuth
37th Swahili Colloquium
Kongamano la Kiswahili litafanyika tena Iwalewahaus (iliyoko Wölfelstr. 2) na litaanza Ijumaa tarehe 30 Mei, saa mbili na nusu asubuhi. Ada ya kiingilio itakuwa Euro 15 (wanafunzi: Euro 10).
Siku moja kabla ya Kongamano kuanza, Alhamisi, tarehe 29 Mei, tutakutana katika mgahawa wa Kithai ‘Hua Hin’ (uliopo Ludwigstr. 30; http://www.thai-huahin.de/) kuanzia saa moja jioni. Tunaomba ufahamu wenu kwamba hatutaweza kutunza bili zenu siku hiyo.
Pia kutakuwa na matukio kadha wa kadha wakati wa kongamano hilo: Tutakuwa na michango ya wanaharakati, wasanii na wageni wa heshima wetu kama mnavyoona kwenye ratiba. Wakati wote wa Kongamano kutakuwepo ‘soko la vitabu’, kwa hivyo mnakaribishwa kuonyesha vitabu vyenu na kufurahia maandishi ya Kiswahili.
Ikiwa una maswali zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana nasi (swahili@uni-bayreuth.de). Tunatazamia kuwakaribisha hapa Bayreuth!
Karibuni sana!